Rais Putin asimamishwa kazi, shirikisho latoa taarifa

 

Shirikisho la Kimataifa la Judo limetoa taarifa ya kumsimamisha kazi Rais wa Urusi, Vladimir Putin kama rais wake wa heshima na balozi, likitaja “mzozo wa vita unaoendelea nchini Ukraine.

Taarifa hiyo inakuja wakati vikosi vya Urusi vikiendelea kushambulia mji mkuu wa Ukrain wa Kyiv na miji mingine, na kusababisha mapigano makali mitaani na kurusha roketi huku na huko.

Shirika la judo, ambalo linamuunganiko wa zaidi ya mashirikisho 200 ya kitaifa, katika taarifa yake iliyotolewa mwishoni mwa wiki imebainisha kuwa limeghairi hafla yake ya Grand Slam huko Kazan, Urusi, ambayo ilipangwa kufanywa Mei.

Rais Putin asimamishwa kazi, shirikisho latoa taarifa Rais Putin asimamishwa kazi, shirikisho latoa taarifa Reviewed by Cadotz media on 6:35 AM Rating: 5

No comments

Comment to Cadotz

Ndugu ahsante kwa kuitembelea Cadotz, Endelea kufurahia huduma zetu pia Tunakusogezea Cadotz uchague unachokitaka katika menyu zetu.
Bofya chini

<<< rudi