Mama atembea na Mume wa mwanae kwa miaka 25

 

Mwanamke mmoja nchini Kenya aitwaye Martha Wanjiku, ameeleza kisa chake, baada ya kubaini mama yake mzazi amekuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na aliyekuwa mume wake kwa zaidi ya miaka 25.

Martha ameeleza kwamba aliolewa na mwanaume huyo na ndoa yao ilidumu kwa miaka miwili pekee na ilipofika mwaka 2020, alibaini mama yake ana mahusiano na aliyekuwa mume wake huyo, alipoenda kuamulia ugomvi baada ya kupigiwa simu na kuambia mama yake anapigwa.

“Nilishtuliwa na simu siku moja asubuhi, nikaambiwa nikaokoe mama yangu anapigwa na mume wangu wa zamani, na nilipomuuliza kwanini anafanya hivyo, aliniambia mtu anaulizwanga akipiga bibi yake?,” alieleza Martha.

Aidha, Martha ameongeza kuwa mama yake alikuwa kwenye mahusiano na mwanaume huyo hata kabla ya wao kuoana na kudai kwamba alishamsamehe lakini hawezi tena kupata ujasiri wa kumtambulisha mama yake hata atakapopata mwanaume mwingine.

Mama atembea na Mume wa mwanae kwa miaka 25 Mama atembea na Mume wa mwanae kwa miaka 25 Reviewed by Cadotz media on 6:25 AM Rating: 5

No comments

Comment to Cadotz

Ndugu ahsante kwa kuitembelea Cadotz, Endelea kufurahia huduma zetu pia Tunakusogezea Cadotz uchague unachokitaka katika menyu zetu.
Bofya chini

<<< rudi