Jeshi la Urusi litawapokea Watanzania waliokwama Ukraine ‘Tokeni kwa Makundi’

 

Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliopo Moscow nchini Urusi umetoa taarifa kwa Wanafunzi wote wa Kitanzania walioko kwenye Chuo cha Taifa cha Sumy nchini Ukraine kwamba Serikali ya Urusi imetengeneza Safe Corridor ya Wanafunzi hao kutoka Ukraine kupitia Urusi kuanzia leo March 05,2022 .

“Wanafunzi wanatakiwa kutoka Chuoni kuelekea eneo la Sudja ambapo watapokelewa na Jeshi la Urusi, kutoka Urusi watasafirishwa na Jeshi hilo hadi eneo la Belgorod ambapo watapokelewa na Maafisa wa Ubalozi wa Tanzania uliopo Moscow kwa taratibu nyingine za kurejea Tanzania”

“Wanafunzi wanashauriwa kutoka Chuoni kwa makundi na kubeba Bendera ya Tanzania ili kuwatambulisha wanapopita kwenye Safe Corridor ili kurahisisha uratibu wa zoezi la mapokezi”

Jeshi la Urusi litawapokea Watanzania waliokwama Ukraine ‘Tokeni kwa Makundi’ Jeshi la Urusi litawapokea Watanzania waliokwama Ukraine ‘Tokeni kwa Makundi’ Reviewed by Cadotz media on 11:15 PM Rating: 5

No comments

Comment to Cadotz

Ndugu ahsante kwa kuitembelea Cadotz, Endelea kufurahia huduma zetu pia Tunakusogezea Cadotz uchague unachokitaka katika menyu zetu.
Bofya chini

<<< rudi