Wasichana Waliojiunga Kikundi Cha Islamic State Waonekana
Kanda ya Video ya CCTV imeonyesha picha za wasichana watatu wa Uingereza waliotoroka nchini kwao kuelekea nchini Syria ili kujiunga na wapiganaji wa IS.
Wasichana hao ambao ni Shamima Begum,Amira Abase wenye umri wa miaka 15 na kadiza Sultana mwenye umri wa miaka 16 walisafiri kutoka London kuelekea Istanbul tarahe 17 mwezi Februari.
Picha hizo zimewaonyesha wakisubiri katika kituo cha basi cha Bayrampasa baadaye siku hiyo. Wapepelezi wa Scotland Yard wanaamini wanafunzi hao wa shule ya Bethnal Green Academy wameingia nchini Syria.
Inadaiwa kuwa wasichana hao wamepelekwa karibu na kivuko cha mpaka huo na wapiganaji hao wa Islamic State. Katika kanda hiyo ya video Inaonyesha kuwa wasichana hao walikaa katika kituo cha basi kwa kwa takriban saa 18.
Wasichana Waliojiunga Kikundi Cha Islamic State Waonekana
Reviewed by Unknown
on
12:25 PM
Rating:
Reviewed by Unknown
on
12:25 PM
Rating:






Post a Comment