NOKIA 105 yatajwa kuwa simu inayotumiwa zaidi na wanamgambo wa kikundi cha Islamic State (ISIS)


Hizi ni baadhi ya sababu kwa nini ISIS wanatumia Nokia 105 kama remote za kulipulia mabomu:

  • Simu ya Nokia 105 ni simu inayoweza kuhimili mikiki mikiki (durable) ya aina yote, ni simu imara zaidi sokoni kwa sasa kwa simu za kawaida (basic phones), ikiwa na bei rahisi zaidi na battery linalokaa na chaji muda mrefu zaidi hivyo inawapa ISIS kila sababu ya kuifanya chaguo lao la kwanza.
  • Simu hiyo inayotumiwa zaidi na magaidi huko Iraq, haina uwezo wa kuinstall apps zozote zile na wala haina kamera hivyo inakuwa ngumu sana kwa wadukuaji wa kimataifa kuidukua simu hii kirahisi.
  • Urahisi wa kutumia simu hii inafanya iwe chaguo la kwanza pale suala la kulipua mabomu linapokuja, njia rahisi ni kuwa na simu mbili, moja inategwa na bomu na nyingine anakuwa nayo mlipuaji, mlipuaji anachofanya ni kuipigia ile simu iliyotegwa na bomu ambayo imeunganishwa na sakiti (circuit) ya bomu, hivyo pale simu inapoingia tu umeme unaruhusiwa kupita katika sakiti ya bomu na kulipua bomu lilotegwa.
  • Linapokuja suala la vibration (mtikisiko) pale inapopigwa Nokia 105 ndio chaguo sahihi, kwani simu hii ina vibration kali zaidi hivyo kusaidia kulipua mabomu kirahisi.
  • Inaonekana wanamgambo wa kikundi cha ISIS wamegundua njia ya kupata simu hizi kirahisi zaidi, kwa kuziiba mtaani au kwa kununua katika mafungu makubwa.
  • Urahisi wa kutoa mafunzo kwa wanamgambo wengine zaidi wa ISIS, simu hizi ni rahisi zaidi kutumia kwenye kutengeneza bomu kuliko simu nyingine yoyote.
Ilikuwa ni rahisi zaidi ISIS kupata simu hizi kwa wingi kwa sababu hazikuwa na nguvu kwenye soko la simu la sasa lililotawaliwa na smartphones. Pia simu hii imetoka katika kipindi ambacho kampuni ya Nokia inaingia mkataba wa kimauzo na kampuni ya Microsoft hivyo kunawapa nafasi ndogo Microsoft kufuatilia simu hizi kwa makini zaidi.


Toa maoni yako

NOKIA 105 yatajwa kuwa simu inayotumiwa zaidi na wanamgambo wa kikundi cha Islamic State (ISIS) NOKIA 105 yatajwa kuwa simu inayotumiwa zaidi na wanamgambo wa kikundi cha Islamic State (ISIS) Reviewed by Unknown on 12:18 PM Rating: 5

No comments

Comment to Cadotz

Ndugu ahsante kwa kuitembelea Cadotz, Endelea kufurahia huduma zetu pia Tunakusogezea Cadotz uchague unachokitaka katika menyu zetu.
Bofya chini

<<< rudi