Raia 300 Wauawa Na Kikundi Cha Islamic State Iraq

Maafisa nchini Iraq wanasema kuwa wanamgambo wa islamic state wamewaua mamia ya watu wa yazidi waliokuwa wakiwazuilia eneo lililo kaskazini mwa nchi.

Makamu wa rais nchini Iraq Osama al-Nujifi ameyalaani mauaji hayo akiyataja kuwa ya kikatili
Taarifa zilisema kuwa hadi watu 300 waliuawa kwenye wilaya moja iliyo magharibi mwa mji wa Mosul siku ya ijumaa.

Wanamgambo wa islamic state walithibiti maeneo yaliyo kaskazini mwa Iraq kwa karibu mwaka mmoja uliopita ambapo waliwaua na kuwashika mateka maelfu ya watu wa Yazidi wakiwaita makafiri.
Raia 300 Wauawa Na Kikundi Cha Islamic State Iraq Raia 300 Wauawa Na Kikundi Cha Islamic State Iraq Reviewed by Unknown on 12:14 PM Rating: 5

No comments

Comment to Cadotz

Ndugu ahsante kwa kuitembelea Cadotz, Endelea kufurahia huduma zetu pia Tunakusogezea Cadotz uchague unachokitaka katika menyu zetu.
Bofya chini

<<< rudi