FAHAMU KUHUSU 'BOKO HARAMU'
Kiongozi wa Boko Haram Abubakar Shekau
• Ilianza 2002
• Kiongozi wake ni Abubakar Shekau
• Takribani watu Milioni 3 wameathirika tangu ianze
• Ilipoanza ilikuwa na lengo la kupinga elimu ya Kimagharibi, elimu ya wazungu - Boko Haram maana yake ni "Elimu ya kimagharibi ni Marufuku/Haram " kwa lugha ya ki ‘Hausa’
• Mwaka 2009 ilianza rasmi mapigano ili kuunda nchi ya Kiislamu
• 2009: Mamia waliuwawa Boko Haram walipovamia kituo cha Polisi cha Maiduguri; Kiongozi wao Mohammed Yusuf alikamatwa na kuuliwa
• Dec 2010: Walilipua Jos na kuua watu 80; ililalamikiwa kwa shambulizi la mkesha wa mwaka mpya katika baraksi ya Abuja
• Aprili 2012: Shambulizxi la mauaji siku ya pasaka huko Kaduna; ofisi za gazeti la Thisday ilipigwa mabomu
• Mei 2013: Boko haramu waliingia fulu masinondo kwenye mji wa Bama na kufanya hari ya hatari itangazwe na serikali
• Sept 2013: Boko wavamia sekondari ya Kilimo ya Yobe naa kuua wanafunzi wa kiume 50
• Machi 2014: mgambo wa Boko walivamia kambi kadhaa za Wanajeshi huko Maiduguri
• Aprili 2014: Walalamikiwa kuuwa takribani atu 75 huko Abuja
• Aprili 2014: Wateka zaidi ya wasichana 200 kutoka kwenye shule iitwayo Chibok iliyopo Jimbo la Borno
• Serikali ya US imetangaza dau la USD 7M (Sh. 11.7 Bilioni) kwa kutoa taharifa za kiongozi wa kundi hili. (NB Marekani ilitangaza dau la USD 25M kwa kutoa habari zitakazowezeshankukamatwa Sadam Hussein)
Abubakar Shekau ni kiongozi wa kundi hili la Wanamgambo wa Kiislamu wanaojiita Boko Haramu, kundi la upinzani lililo nyuma ya mauaji upande wa Kaskazini Mashariki mwa Nigeria kwa miaka 5 sasa.
Wafuasi wa kundi hili wanasemekana wamehamasishwa na haya za Korani zinazosema “Yeyote asiye simamiwa na ufunuo wa Mungu ni kati ya wenye dhambi”
Boko Haram inahamasisha mwenendo unaoitwa wa Kiislamu unaotambua “Haramu” au Katazo kwa waislamu kushiriki katika shughuli za kisiasa au shughuli za kijamiii zinazohusiana na utamaduni wa kimagharibi.
Hii inajumuisha na upigaji wa kura kwenye uchaguzi, uvaaji wa shati na suruali au kupata elimu kwenye shule zinazofuta mfumo wa elimu wa kimagharibi/elimu dunia (Secular education).
Boko Haramu wanatambua Serikali ya Nigeria kuwa inaendeshwa na wasioamini dini, pamoja na kuwa nchi ina rais mwislamu.
"Kundi hili jina lake hasa ni Jama'atu Ahlis Sunna Lidda'awati wal-Jihad hiki ni kiharabu na maana yake ni “Watu wenye msimamo wa kueneza mafundisho ya mitume na Jihad”
Mafunzo ya wafuasi
Ni wakazi wa Maiduguri mji uliopo Kaskazini Mashariki, sehemu ambayo kuna makao makuu ya Jama'atu Ahlis Sunna Lidda'awati wal-Jihad ndio walioibatiza na kuita Boko Haramu.
Kwa uhalisia neon Boko linamaanisha ‘isio halisi’ (fake) lakini neon hili likaja kuhusishwa na elimu ya magharibi, na Haram inamaana ‘iliyozuiwa’ au kukatazwa.
Tangu enzi za Khalifa wa Sokoto aliyetawala sehemu ambazo kwa sasa ni Kaskazini mwa Nigeria, Niger and Kusini mwa Cameroon, maeneo yaliyokuja kuangukia kwenye utawala wa Ukoloni wa Waingereza mnamo 1903, kumekuwepo na ukinzani kwenye baadhi ya sehemu kwa waislamu kupinga elimu ya Magharibi.
Wanakataa kuwapeleka watoto wao kwenye shule za serikali “shule za kimagharibi” tatizo lililojengwa na viongozi wao wanaoona elimu sio kipaumbele.
Mazingira haya ndiyo yaliyomfanya kiongozi huyu mwenye uwezo wa ushawishi na muislamu Mohammed Yusuph kuunda kundi la Boko Haram huko Madiguri 2002. Ametengeneza taasisi kubwa ya kidini inayojumuisha msikiti na shule za kiislamu.
Familia za Wasilamu wengi walio masikini kutoka sehemu mbalimbali za Nigeria na nchi za jirani, wamewapeleka watoto wao kwenye shule hizi.
Boko haramu sio tu inatoa huduma za shule, bali lengo lake la msingi ni kuwa na nchi ya kiislamu, na shule hizi zimekuwa sehemu za kutoa mafunzo za jihadi.
Jeshi la Nigeria liliweza kuvamia makao makuuu ya Boko na kukamata wapiganaji wake na kumuua Mr Yusuf mwanzilishi wake.
Mwili wake ulionyeshwa kwenye TV ya taifa na maafisa wa jeshi wakatangaza kuwa Boko Haramu imeshasambaratishwa.
Wapiganaji hawa baadae wakajikusanya upya chini ya kiongozi wao wa sasa Abubakar Shekau na kuendelea na upinzani.
Mnamo 2010 US ikaitangaza kuwa taasisi ya Kigaidi, kutokana na hofu kuwa imetengeneza mtandao na makundi mengine ya wanamgambo kama vile al-Qaeda ili kufanya jihadi dunia mzima.
Boko Haramu staili yao mwanzoni ilikuwa ni kutumia pikipiki huku wakiwa na bunduki, huku wakiua polisi, wanasiasa na yeyote anayepinga falsafa zao ikiwa ni pamoja na waislamu kutoka kwenye makundi mengine na wachungaji wa kikristo.
Kundi hili limefanya mashambulizi ya kuogofya kaskazini mwa Nigeria, ikiwa ni pamoja na ulipuaji wa mabomu kwenye makanisa, kwenye mabasi, kwenye sehemu za starehe, kambi za jeshi, polisi, makao ya UN na mji mkuu wa Abuja.
Kutokana na ukuaji wa uhalifu huu wa Boko, rais Goodluck Jonathan akatangaza hali ya hatari mei 2013 katika majimbo matatu ya kaskazini mwa Nigeria huko Borno, Yobe na Adamawa, sehemu ambazo Boko wananguvu.
Boko inapata zaidi wapiganaji wake kutoka kabila la Kanuri, ambalo ni kubwa kwenye majimbo haya 3. Wakanuri wana alama maalumu ya mabaka kama wanavyofanya wamakonde, na kutokana na matamshi yao ya lugha ya ki hausa inakuwa rahisi kutambulika na wanigeria.
Kutokana na hali hii wanamgambo wamekuwa wakifanya shughuli zao maeneo ya kaskazini mashariki kama eneo lao la kujidai na eneo wanalolijua vizuri.
Umaskini wa Kutupwa
Upelekaji wa majeshi kuwakabili Boko Haram umewafukuza na kuiacha Maduguri, ngome yao kuu ya mjini na wameelekea kwenye msitu wa Sambisa msitu uliopo kwenye mpaka kati ya Nigeria na Cameroon.
Wakiwa kule makundi ya Boko yameweza kuanzisha mashambulizi ya halaiki kwenye vijiji, uharibifu wa mali, wamechoma moto mali na nyumba kama njia yao ya kuwatahadharisha watu wa vijijini kutoshirikiana na majeshi ya serikali kama ambavyo wananchi wa Miduguri walivyofanya.
Boko Haramu pia ilifanya harakati zake za kuonyesha kutokukubaliana na elimu ya kimagharibi, elimu ambayo wanaamini imevunja maadili ya kiislamu hasa kwa watoto wa kike kwa kuvamia shule mbili za bweni za wasichana, mwezi wa 3 huko Yobe na mwezi wa 4 huko Chibok.
Boko wameteka zaidi ya wasichana 200 wa shule huko Chibok na wamedaia kuwa watawafanyya watumwa na kuwaoa, kama rejea ya imani ya Kiislamu ya kale inayoamini kuwa mwanamke aliyekamatwa kwenye mapigano ni sehemu ya vitu vya kujilipa kwenye vita ‘’war booty’’
Boko walileta tishio kama hili mei 2013, walipotoa kideo inayosema tumechukua wanawake na watoto ikiwa ni pamoja na wasichana ili kujibu kitendo cha kuchukuliwa wake na watoto wa wenzetu. Hili lilisuluhishwa kwa kubadilishana wafungwa kwa pande zote na wanawake na watotoi wakaachiwa.
Wakati huohuo Boko Haram wameendelea na kampeni yao ya kushambulia maeneo ya mijini, kwa kulenga mji mkuu hapo Aprili kwa kusababisha mauaji ya watu 70 kwenye mlipuko uliotokea karibu na sehemu ya kupaki magari, tukio lingine lilitokea mei 2 watu 19 walipoteza maisha.
Hii inaonyesha ni namna gani Boko Haram walivyokuwa na maelfu ya majeshi ya kupigana, lakini pia inaonyesha ni kwa kiasi gani ilivyo mahiri kwa utengenezaji wa mabomu.
Wachambuzi wa mambo wanasema kuwa Nigeria ya kaskazini ina historia ya kuzalisha makundi ya wanamgambo wa kiislamu, Boko Haramu imeonekana kwenda mbele zaidi na kuwa kinara wa kuwazalisha na imedhibitisha kuwa kikundi hatari zaidi kikija na ajenda yake ya Jihad vita takatifu ya kiislamu kuwapinga wasiokuwa waislamu.
Tishio hili linaweza kupungua sana na kuondoka endapo serikali ya Nigeria itaweza kupunguza umaskini uliokithiri kwenye mikoa mbalimbali na kujenga mfumo wa elimu unaokubalika na jumuiya ya kiislamu, wachambuzi walisema.
Kiongozi wa Boko Haram: Abubakar Muhammad Shekau
Abubakar kiongozi wa Boko anasemekana kuwa ni mtu aliuyejitenga asiyekuwa na uoga, mtu asiyefahamika vizuri, mtu aiyetabirika, sehemu moja yeye ni mwenye elimu ya dini na sehemju nyingine ni mhuni.
Tangu alipochukua uongozi wa Boko Haram amekuwa na siasa kali sana na amekuwa akiratibu mauaji mengi zaidi tofauti na kabla ya kuwa kiongozi.
Huenda moja ya mambo aliyoyafanya ya kushtusha ni pale alipotoa video akicheka na alipodhibitisha kuhusika na utekaji wa wasichana wa shule zaidi ya 200, akitoa ahadi ya kuwauza.
"Nimewateka wasichana wenu, nitawauza sokoni kwa msaada wa Allah, nitawauza na kuwaoa."
Kwa uoendo mkubwa anaitwa na wafuasi wake kama Imam au Kiongozi. Abubakar Muhammad Shekau amezaliwa kijiji cha Shekau kilichopo Kaskazini mashariki mwa Nigeria katika Jimbo la Yobe.
Baadhi wanasema ana umri wa miaka 30 na kitu hivi, wengine wanasema yupo kwenye maiaka 40 ya katikati, kutokuwa na uhakika wa umri unaiongeza sintofahamu iliyomzunguka
.
Mwanafunzi wa dini ya siasa kali
Shekau aliwahi kutangazwa kuwa ameuwawa kwa majeshi ya usalama 2009. Mwaka mmoja baada ya tukio hili alionekana tena kwenye video kama kiongozi mpya wa Boko Haram. Malalamiko ya aina hii hii yaliwahi kutokea tena kuwa amefariki na ikaja kudhibitishwa baadae kuwa siyo kweli.
Mwanzilishi wa Boko, Muhammad Yusuf, alifariki akiwa ameshikiliwa na polisi Jul 2009 na wengi waliuwawa kwenye operesheni ya kuwatafuta, operesheni ambayo wengi wanalaumu inafanya kikundi hiki kuleta fujo zaidi. Tangu kipindi hicho Shekau hajawahi kuonekana kwenye hadhara.Badala yake ni picha na video zimekuwa zikitolewa mara kwa mara kupitia mtandaoni.
“Nina jisikia vizuri kuua kila mtu
Niliyeagizwa kufanya hivyo na Mungu”
Abubakar Shekau Boko Haram leader
"Nina penda kuwa watu kama ninavopenda kuua kuku na kondoo” alisema kwenye video aliyoitoa baada ya mauaji waliyoyafanya Jan 2012 kwa kuua watu 180 huko Kano, mji mkubwa kwa kaskazini mwa Nigeria
Shekau anafaahaamu vizuri lugha ya Kanuri, pia anafahaamu Ki Hausa na Ki Arabu. Anafahamu pia kuweka kiingereza kwenye kanda za video wanazozitoa kwa waandishi wa habari.
“Ni mara chache sana anaongea,
Haogopi kitu”
Wakati Muhammad Yusuf anafariki, inasemekana Shekau alioa mmoja ya wake zake 4 na karidhi watoto, huenda kwa mujibu wa vyanzo hii ilifanyika ili kulinda ukaribu na kufanya utakaso.
Kundi la Boko inasemekana halina uongozi wa sehemu moja (decentralize structure) na Shekau hawasiliani na askari wa miguu mojakwamoja bali kupitia viongozi wachache wwaliochaguliwa, hata hivyo hukutana kwa nadra.
" Walio wengi wanaofahamika kama viongozi katika makundi tofautitofauti hawana mawasiliano naye ya mojakwamoja”
Shekau hana mvuto na wala hana umahiri wa kuongea kama kiongozi aliyepita, hata hivyo anasimamia itikadi zake vizuri na ni katili, hii imesemwa na wanaofanya utafiti kuhusu kundi hili.

Reviewed by Unknown
on
1:46 PM
Rating:

Post a Comment