Washukiwa wa al-Shabaab watiwa mbaroni Nyamira

Maafisa wa polisi katika Kaunti ya Nyamira wamewatia mbaroni wanaume wawili wanaoshukiwa kujihusisha na kikundi cha ugaidi cha al-Shabaab.
Wawili hao walitiwa mbaroni siku ya Jumanne baada ya kupatikana wakipiga picha jengo la benki ya Equity na lile la benki ya Family katika mji wa Nyamira.
Akitibithisha kisa hicho mkuu wa polisi katika Kaunti ya Nyamira, Carim Mwandoe alisema baada ya uchunguzi wawili hao walishukiwa kuwa kwa kikundi cha al-Shabaab.
Akizungumza na waandishi wa habari katika mji wa Nyamira, Mwandoe alisema wawili hao walipatikana na picha zingine ambazo ni za ofisi ya kamishena wa kaunti hiyo.
Aidha, afisa huyo alisema kuwa uchunguzi ulibaini kuwa mmoja wao ni wa asili ya Kisomalia na anaishi katika eneo la Eastleigh mjini Nairobi, na wapili anatoka jamii ya Kisii na anaishi Mombasa.
“Hawa wawili tutaendelea kuwachunguza kwa kina maana si watu wa kawaida,” alisema Mwandoe. 
Wawili hao walichukuliwa hadi kituo cha polisi cha Nyamira huku uchunguzi wa kina ukiendelea kufanywa dhidi yao kubaini ukweli wa mambo.
Washukiwa wa al-Shabaab watiwa mbaroni Nyamira Washukiwa wa al-Shabaab watiwa mbaroni Nyamira Reviewed by Unknown on 1:53 PM Rating: 5

No comments

Comment to Cadotz

Ndugu ahsante kwa kuitembelea Cadotz, Endelea kufurahia huduma zetu pia Tunakusogezea Cadotz uchague unachokitaka katika menyu zetu.
Bofya chini

<<< rudi