Vijana 85 Waliojiunga Na Al Shabaab Wajisalimisha

Kufuatia serikali ya Kenya kutangaza kuwasamehe vijana waliojiunga na wananmgambo wa Alshabaab  hatimaye takriban vijana 85 wamejisalimisha kwa jeshi la polisi nchini Kenya.
Vijana hao wamejisalimisha kwa serikali ya Kenya, ili kupokea msamaha uliotelewa kwa wale wote ambao wamepokea mafunzo ya itikadi kali ya kiislamu na kujiunga na kundi la wapiganaji wa Al-Shaabab.
Msemaji wa Serikali imesifu hatua ya vijana hao, akitaja kuwa itachangia  ukusanyaji wa taarifa za kijasusi. Awali vijana hao walihofia kujisalimisha kwa hofu kuwa wangetengwa katika jamii na hata kufungwa gerezani.
Serikali ya Kenya iliahidi kuwasamehe vijana hao mapema mwezi uliopita, kufuatia uvamizi katika chuo kikuu cha Garissa, ambapo zaidi ya watu 150 waliuawa.
Maafisa katika wizara ya mambo ya ndani wamesema kuwa vijana hao walikuwa kati ya umri wa miaka ishirini na thelathini.
Kujasalimisha kwa vijana hao kumepiga jeki juhudi za serikali ya Kenya dhidi ya mafunzo ya itikadi kali, yanayochangia hatua ya vijana hao kujiunga na makundi ya kivita kama vile Al Shabab.
Vijana 85 Waliojiunga Na Al Shabaab Wajisalimisha Vijana 85 Waliojiunga Na Al Shabaab Wajisalimisha Reviewed by Unknown on 2:34 PM Rating: 5

No comments

Comment to Cadotz

Ndugu ahsante kwa kuitembelea Cadotz, Endelea kufurahia huduma zetu pia Tunakusogezea Cadotz uchague unachokitaka katika menyu zetu.
Bofya chini

<<< rudi