Tanzania Yachukua Tahadhari Dhidi Ya Al Shabaab

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Imesema kuwa ipo katika tahadhari dhidi ya uwezekano wa kushambuliwa kikundi cha ugaidi katika miji ya Dar es salaam na Mwanza.
Kwa mujibu wa  waziri wa Mambo ya ndani Mathias Chikawe amesema kwamba nchi  ipo katika tahadhari ya juu kufuatia taarifa za vyombo vya habari kuripoyi kwamba, kuna uwezekano wa shambulio la ugaidi katika miji ya Dar es salaam na Mwanza.
Hatua inafuatia   baada ya taarifa zilizo bainisha kuwa mmoja ya waliokamatwa katika shambulio la chuo kikuu cha Garissa nchini Kenya ni Mtanzania. Mpaka sasa serikali ya Tanzania haijaweza kudhibitisha ripoti zinzaoenea, kuhusu shambulio la ugaidi nchini humo.
Pamoja na hayo waziri Chikawe amesema kuwa serikali ya Tanzania, inafahamu kuwa mmoja ya watuhumiwa walikokamatwa huko Garissa Kenya ni Mtanzania. Amesema watawasiliana na polisi wa Kenya wakimaliza kumhoji mtuhumiwa huyo.
Kwa upande mwingine Tanzania  imewahi  kukumbwa na shambulio la ugaidi mwaka 1998 wakati mabomu yalilipuka katika balozi za Marekani, jijini Dar es salaam na Nairobi, Kenya na kusababisha vifo ya watu wengi.
Tanzania Yachukua Tahadhari Dhidi Ya Al Shabaab Tanzania Yachukua Tahadhari Dhidi Ya Al Shabaab Reviewed by Unknown on 2:30 PM Rating: 5

No comments

Comment to Cadotz

Ndugu ahsante kwa kuitembelea Cadotz, Endelea kufurahia huduma zetu pia Tunakusogezea Cadotz uchague unachokitaka katika menyu zetu.
Bofya chini

<<< rudi