Lady Jay dee' Aeleza juu ya Umiliki wa EFM Radio 93.7

Maswali yamekuwa mengi kwa mwimbaji mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva hapa nchin Judith Wambura 'Lady Jaydee' juu ya maisha yake ambapo aliulizwa juu ya kuachana na mumewake lakini pia kuhusiana na kufungua kituo cha matangazo kwa njia ya sauti (Radio) na au umiliki wa EFM Radio inayo patikana kwenye masafa ya 93.7 Fm jijini Dar es Salaam.
Haya ndiyo aliyo sema kupitia account yake ya Instagram.

Ulituahidi utafungua Radio mbona kimya mpaka leo?
JIBU : "Niliandika hiyo kitu siku ya wajinga duniani, April 1, sikuwahi kuahidi.
Lakini matamanio yangu ni siku moja kumiliki kituo cha radio na ikibidi hata television.
Hakuna linalo shindikana, palipo na nia.EFM radio ni yako?
JIBU : Hapana sio yangu
Nafikiri inadhaniwa hivyo kutokana na kila mtu ku tamani, mimi niwe na radio.
Je!mtaniruhusu na mimi niwaulize swali?
Kwanini mnatamani sana niwe na radio? ?
Mungu akijaalia ntakuwa nayo " Ameandika Lady JayDee.
Baada ya kutangaza kuwa kwa sasa yuko single, miongoni mwa maswali ambayo Lady Jaydee amekutana nayo ni kuhusu sifa za mwanaume ambaye anamtaka awe mpenzi wake kwa sasa.
Kupitia Instagram Jide aliorodhesha sifa za mwanaume amtakaye kwa sasa, soma huenda ukawa nazo (kama wewe ni mwanaume mwenye ndoto za kuwa na staa huyo).



Yapo maswali mengine pia ambayo yanahusiana na mahusiano ambayo ameyajibu.

“SWALI: Mwanaume mwenye vigezo gani ungependa kuwa nae kwa sasa?
JIBU : Anaejali na kuheshimu, mwenye roho ya upendo na huruma, anaeweza ku take care of me financially.
Asiechepuka hovyo (Milupo kila kona )
Asiwe tegemezi
Hata km sio tajiri lakini asinitegemee
Asiwe mlevi kupindukia wa kulala bar ,
Wala kulala nje kwa machangu wa Kinondoni au popote pale
Nikikohoa tu awepo hapo

SWALI: Una boyfriend sasa hivi? 
JIBU : Nashindwa kutofautisha boyfriend na lover, wanaojua kizungu wanaweza kunisaidia.
Ila kama ni kwa maana ya rafiki wa kawaida wa kiume,
Nina boyfriends not boyfriend By the way, marafiki zangu wengi ni wanaume zaidi kuliko wanawake. Kama nimeielewa kwa maana hiyo ninayodhania mimi.
Ila kama sio maana hiyo, sina boyfriend then.

SWALI: Eti una boyfriend mzungu?
JIBU : Nina marafiki wa kiume kadhaa ambao sio raia wa hapa, wenye ngozi tofauti na yangu, urafiki wetu ni wa kubadilishana mawazo, kwenda dinner, ku party kiaina na kualikana ma nyumbani kufungua Champagne na kuchoma nyama.
Kama mmeniona nao huko, we were just having fun, nothing serious.
Na sehemu nnazo kuwa nao ni kwenye mkusanyiko wa watu wenye jinsia tofauti.
Not in a bedroom.

SWALI: Una mpenzi kwa sasa? 
JIBU : Ndio, ninae mpenzi kwa miaka mingi sana.
Ananipa karibia kila nnachotaka,
Amenijengea nyumba
Ameninunulia viwanja
Ameninunulia magari
Ananilisha na kunivisha
Anasomesha ndugu zangu
Amenifungulia restaurant Na ameahidi kuninunulia Beach House, na Land Rover model ya 2015.
Ila hizo ni ahadi, bado hajazitimiza.
Kila nikitaka kwenda holiday anagharamia kila kitu
Nikikohoa nataka kwenda kwa fasi ya Paris ana lipa
Tena ananilipiaga ndege business class
Sasa hivi ameniahidi kunilipia trip ya Italy nikawaone kina Kayumba….Ma shopping n.k Hajawahi kunisaliti
Jina lake anaitwa MUZIKI

Maswali yote yanahusu mapenzi / mahusiano lakini nafikiri hayahusiani na ndoa,
Hivyo swala la ndoa naomba nilitenge nitalijibu Ijumaa / Friday ndio litakuwa no. 10 na la mwisho Vipi kwani, mbona wengine mnasonya?”
Lady Jay dee' Aeleza juu ya Umiliki wa EFM Radio 93.7 Lady Jay dee' Aeleza juu ya Umiliki wa EFM Radio 93.7 Reviewed by Unknown on 10:46 AM Rating: 5

No comments

Comment to Cadotz

Ndugu ahsante kwa kuitembelea Cadotz, Endelea kufurahia huduma zetu pia Tunakusogezea Cadotz uchague unachokitaka katika menyu zetu.
Bofya chini

<<< rudi