Mazungumzo ya amani ya Urusi na Ukraine yaanza

 

Siku ya tano baada ya majeshi ya Urusi kuingia Ukraine, wajumbe kutoka nchi hizo mbili wameanza mazungumzo yenye lengo la kumaliza vita.

Ofisi ya rais wa Ukraine inasema inataka kusitishwa mara moja kwa mapigano na kuondolewa kwa vikosi vya Urusi.

Wakati huo huo Moscow inataka kufikia makubaliano ambayo yalikuwa kwa maslahi ya pande zote mbili, kulingana na mpatanishi wa Urusi, Vladimir Medinsky.

Kabla ya mkutano huo kuanza, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky aliwataka wanajeshi wa Urusi kuweka chini silaha zao, na kutoa wito kwa EU kuipatia Ukraine uanachama wa umoja huo mara moja

Mazungumzo ya amani ya Urusi na Ukraine yaanza Mazungumzo ya amani ya Urusi na Ukraine yaanza Reviewed by Cadotz media on 6:07 AM Rating: 5

No comments

Comment to Cadotz

Ndugu ahsante kwa kuitembelea Cadotz, Endelea kufurahia huduma zetu pia Tunakusogezea Cadotz uchague unachokitaka katika menyu zetu.
Bofya chini

<<< rudi