Uganda: mbunge apigwa faini kwa kukojoa hadharani


Mahakama Jijini Kampala nchini Uganda, imemtoza faini ya Shilingi za uganda 40,000 sawa na Shilingi za Kitanzania 24,500 Mbunge Abraham Abiriga baada ya kusambaa kwa picha katika mitandao ya kijamii zikimuonyesha akikojoa kwenye ukuta wa jengo karibu na wizara ya fedha nchini humo.
Mbunge huyo ameshtakiwa chini ya sheria ya jiji inayoeleza ikiwa mtu yeyote anapatikana na hatia ya “kuimarisha mjini” au kusababisha shida kwa umma atatozwa faini ya shilingi za uganda 40,000 au adhabu ya kifungo jela miezi miwili au vyote viwili.
Mbunge Abiriga alipohojiwa na mwandishi wa habari kutaka kujua ni kwa nini alifanya kitendo hicho alijitetea kwa kusema “Kwa nini nibaki na mkojo?”
Uganda: mbunge apigwa faini kwa kukojoa hadharani Uganda: mbunge apigwa faini kwa kukojoa hadharani Reviewed by Unknown on 3:45 PM Rating: 5
Ndugu ahsante kwa kuitembelea Cadotz, Endelea kufurahia huduma zetu pia Tunakusogezea Cadotz uchague unachokitaka katika menyu zetu.
Bofya chini

<<< rudi