CHADEMA:Tumepokea kwa masikitiko taarifa za mauaji yanayoendelea kibiti

Mwenyekiti waCHADEMAna Kiongozi Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani BungeniFreeman Mboweameonesha kusikitishwa na mauaji yaraia wasiokuwa na hatia yanayoendelea katika maeneo yaKibiti,MkuranganaRufiji.Akizungumzia msimamo waCHADEMAjuu ya mauaji hayoMboweamesema chama hicho kinaingana na kinachotokea Mkoa waPwani.“Kinachoendelea Mkuranga, Kibiti na maeneo mengine ya Mkoa wa Pwani. Hatuungi mkono mauaji ya raia na viongozi. Hilo naomba niliweke wazi sisi kama chama. Hatuungi mkono mauaji ya viongozi bila kujali wanatoka chama gani au bila kujali wanatoka Serikali ipi au wana wajibu gani wala raia yeyote wa nchi yetu. Hatuungi mkono na tunalaani sana mauaji yanayoendelea.”Aidha, amesema wanasikitika na namna Serikali inavyolichukulia suala hilo akiwataka viongozi wa kisiasa kuviachia vyombo vya Ulinzi na Usalama vifanye kazi yake.“Tunasikitika na namna ambavyo Serikali ya Awamu ya Tano inavyoshughulika na jambo hili. Kauli za viongozi wetu mbalimbali za majigambo zinaonekana kuwachochea wauaji kwa sababu linapotoka tamko lolote la majigambo anakufa mtu usiku ama anakufa mtu kesho yake. Viongozi wetu wa kisiasa waachie vyombo vyaUlinzi na Usalama vifanya kazi. Matamko mengi yanatolewa na viongozi wetu wa kisiasa. Hatuna hakika ni nini kinaendelea.” Katika kutafuta suluhisho zaidi juu ya tatizo la mauaji ya Pwani, Mbowe amevitaka Vyombo vya Ulinzi na Usalama kutumia ujuzi wa ziada kukabiliana na wauaji ikiwa pia kuwashirikisha watu mbalimbali na taasisi mbalimbili.“Tunataka Majeshi yetu na vyombo vyetu vya Ulinzi na Ulasama vitumie weledi wa ziada. Sio kila wakati nguvu tu inaweza ikasaidia. Busara nyingine zote zitumike; Wazee watumike, Vyombo vya Serikali vitumike, Viongozi wa Kidini watumike.”– Freeman Mbowe.Walichosema Lema na Mnyika kuhusu mauaji ya Kibiti Bungeni!!!
CHADEMA:Tumepokea kwa masikitiko taarifa za mauaji yanayoendelea kibiti CHADEMA:Tumepokea kwa masikitiko taarifa za mauaji yanayoendelea kibiti Reviewed by Unknown on 11:28 PM Rating: 5

No comments

Comment to Cadotz

Ndugu ahsante kwa kuitembelea Cadotz, Endelea kufurahia huduma zetu pia Tunakusogezea Cadotz uchague unachokitaka katika menyu zetu.
Bofya chini

<<< rudi