Mwanafunzi aliyefanyishwa ngono siku nne mchana na usiku asema, "Nilikiona kifo kileee!"
MWANAFUNZI wa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Marangu inayomilikiwa na kanisa Katoliki jimbo la Moshi, (jina limehifadhiwa) alitekwa na kukufungiwa kwenye hoteli moja ya kitalii mjini hapa na kufanyiwa vitendo vya ngono kwa muda wa siku nne mfululizo.
Mwanafunzi huyo anadaiwa kutekwa Agosti 6 mwaka huu na kijana mmoja (jina linahifadhiwa) mfanyakazi wa kampuni ya simu za mikononi (Airtel) mjini Dodoma. Akizungumza jana na Tanzania Daima Jumatano, kaka wa mwanafunzi huyo, Joseph Temba, alidai mdogo wake alitekwa na mtu huyo na tayari mtuhumiwa ameshakamatwa. Alisema walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo Agosti 10, mwaka huu, katika baa moja akiwa na mdogo wake baada ya raia wema kutoa taarifa za kuonekana kwake.Kwa mujibu wa kaka wa mwanfunzi huyo siku ya tukio alipokea simu kutoka kwa mwangalizi wa wanafunzi (matroni) akimjulisha kutokuwapo bwenini kwa mdogo wake na ndipo walipoanza kufuatilia na kutoa taarifa kituo kikuu cha polisi mjini Moshi na kupewa namba Mos/RB/9196/2013.
You might also like:
Mwanafunzi aliyefanyishwa ngono siku nne mchana na usiku asema, "Nilikiona kifo kileee!"
Reviewed by Unknown
on
2:52 PM
Rating:
Post a Comment